Sunday, 3 November 2013

Sonko Kufika mbele ya kamati za uchunguzi ya Westgate

Seneta wa Kaunti ya Nairobi, Mike Mbuvi


Seneta wa Kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi ''Sonko''anatarajiwa kufika mbele ya kamati za bunge, zinazochunguza shambulizi la Westgate.

Sonko anatazamiwa kuhojiwa kuhusu madai yake kwamba idara ya usalama imezembea katika kazi yake. Kamati ya Bunge Kuhusu Utawala na Usalama wa Taifa na ile kuhusu Ulinzi na Mashauri ya Nchi za Nje, zinatarajiwa kuanza kupokea maoni kutoka kwa wananchi Jumatatu wiki ijayo. Mwenyekiti wa kamati ya Utawala na usalama Asman Kamama amesema tayari wakenya watatu wameziambia kamati hizo kwamba wako tayari kutoa maoni.

Kamama amesema kamati hizo pia zitafanya uchunguzi kuhusu madai ya maafisa wa usalama kutekeleza wizi katika Jumba la Westgate wakati wa shughuli ya uokoaji. Amesema wale watakaopatikana na hatia watachukuliwa hatua kwa mujib wa sheria.

Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa hatua ya rais kutangaza kubuniwa kwa kamati itakayochunguza shambulizi la Westgate haitaathiri uchunguzi wao.

Kando na hayo amesema watatembelea kambi za wakimbizi katika maeneo ya Mandera, Garrisa, na Mombasa, ambako mashambulizi ya kigaidi yamekuwa yakitekelezwa katika siku za hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment